NDOA ZA UTOTONI: JINAMIZI LINALOTAFUNA MAISHA YA WATOTO WA KIKE NCHINI
Tanzania ni miongoni mwa nchi nyingi duniani na hasa Afrika ambazo zina kiwango cha chini cha elimu kwa watoto wa kike. Utafiti unaonyesha umasikini na uzalianaji ni vitu vinavyokwenda sambamba, wazazi huzaa watoto wengi kwa ajili ya sababu mbambali ikiwemo kupata nguvu kazi ya shambani na nyumbani. Nchini Tanzania, kwa miaka mingi watoto wa kike wamekuwa wakifanya vizuri kuliko watoto wa kiume, kuanzia miaka ya 1990 wasichana wamekuwa wakifanya vizuri darasani na hata kuongoza katika mitihani ya taifa ya kidato cha nne ikiwepo mwaka 2009 aliongoza Imaculate Mosha, 2013 Robina Nicholaus, 2014 Nyakaho Marungu, 2015 BUtogwa Charles Shija, lakini idadi yao inapungua siku hadi siku, ngazi hadi ngazi. Swali linakuja je, ni wapi watoto wa kike huishia? Mbona ni wachache sana katika ngazi ya juu ya elimu ukifananisha na wavulana? Majibu ni mengi lakini linalo umiza moyo ni kusikia kuwa wasichana wengi husitisha masomo yao ili waolewe.
“majibu ni mengi lakini linalo umiza moyo ni kusikia kuwa wasichana wengi husitisha masomo yao ili waolewe”
Wengi huolewa wakiwa wadogo na kwa msukumo wazazi, wengi wao huishia katikati katika safari yao ya elimu. Huacha shule na kwenda kuolewa na mara nyingi huolewa na watu waliowazidi umri kwa miaka mingi. Wasichana huanza wengi sana ngazi ya msingi lakini hupungua kadri ngazi zinavyoongezeka , mpaka kufikia ngazi ya sekondari wasichana hupungua kwa Zaidi ya asilimia 43 katika shule zetu nyingi. Nchini Tanzania, mikoa inayoongoza kwa ndoa za utotoni ni shinyanga, tabora, mtwara, pwani,Dodoma, Ruvuma, lindi kigoma na sehemu za mbeya vijijini ikiwemo wilaya ya mbarali. Serikali imekazana kukamata mafisadi, wala rushwa, majangili na wasiolipa kodi imesahau wale mafisadi wanaoharibu maisha ya watoto wa kike wengi nchini.
Inaumiza kuona mtoto wa kike mwenye miaka 15 au 16 akiolewa na kuwa mama wa nyumbani, hivi mtoto wa 16 atawezaje kuwa mama wa nyumbani? Mzazi unakubali mtoto wako aolewe akiwa na huo umri hakuna hata
“Wanawake wakiwezeshwa wanaweza pia wakipewa nafasi wanafanya
kweli, mama Asha Rose Migiro alikuwa naibu katibu mkuu wa umoja wa
mataifa, mama Samia Suluhu Hassan ni makamu wa rais na wengi ni mawaziri
katika baraza la mawaziri la hapa nchini”.
|
madhara ya ndoa za utotoni.
wazazi wengi hawajui madhara ya ndoa za utotoni kwa watoto wao, wengi wao
hupata maradhi ya kizazi kwa sababu miili yao ni midogo na maumbile yao bado
hayajafikia kuzaa, ndoa nyingi za
utotoni huvunjika kwa sababu wasichana wengi hawana uzoefu na maisha ya
ndoa na hawakufundwa ipasavyo kwa kuwa ni wadogo, wasichana wengi hufariki wakati wa kujifungua, hiyo ni
kwa sababu ya kutokwa na damu nyingi hivyo kuishiwa damu na hatimaye kupoteza
maisha, watoto wengi wanaozaliwa na wasichana wadogo huzaliwa hawana afya yaani
njiti, wasichana wengi huishia kutanga tanga baada ya kuolewa kwa sababu hawana
kazi ya kufanya na waliacha shule.
Utafiti unaonyesha asilimia kubwa ya wasichana hujutia
kuacha shule na wangetamani kurudi shule kusoma kwa kuwa maisha ni magumu bila
elimu. Katika ndoa za utotoni wanao athirika Zaidi ni watoto wa kike kuliko
wavulana. Wanawake wakiwezeshwa wanaweza pia wakipewa nafasi wanafanya kweli,
mama Asha Rose Migiro alikuwa naibu katibu mkuu wa umoja wa mataifa, mama Samia
Suluhu Hassan ni makamu wa rais na wengi ni mawaziri katika baraza la mawaziri
la hapa nchini. Tunaiomba serikali, wadau mbalimbali, mashirika binafsi na watu
wema kusaidia kukomesha janga hili ili tuokoe kizazi chetu na hatimaye wanaume
waweze kuoa wanawake wasomi na wanaojitambua.
je, serikali haioni hili
jambo au inafumbia macho?
Jamii nyingi za kiafrika na hata zisizo na asili ya afrika kama zile zenye asili ya asia huozesha watoto wao wakiwa wadogo sana kiasi
cha miaka 14 hadi 15, hili huchangiwa pamoja na sheria ya ndoa ya hapa nchini
ambayo katika kifungu cha 13 cha sheria ya ndoa ya mwaka 1971kinachoruhusu
mtoto wa kike kuolewa akiwa na miaka 14 kwa idhini ya mahakama na miaka 15 kwa
idhini ya wazazi. Kwa sharia hii watoto wa kike wengi wataishia kuwa hawana
elimu tosha.
Leave a Comment